YANGA YAPATA USHINDI UWANJA WA TAIFA


Mshambuliaji Donald Ngoma ametuma salamu Msimbazi baada ya kuifungia Yanga bao pekee ikishinda 1-0 dhidi KMKM kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam jana.

Donald Ngoma

Ngoma aliyesajiliwa akitokea Platinum ya Zimbabwe alisubiri hadi dakika ya 50 kufunga bao lake la kwanza Yanga akiunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Andrey Coutinho.

Baada ya kufunga bao hilo Ngoma alikimbia hadi kwenye jukwaa walilokaa mashabiki wa Simba ambao walikuwa wakimzoea muda mrefu na kuonyesha ishara ya kuwataka watulie.
Share on Google Plus

About Habari Duniani

WELCOME TO MICHEZOTU (SPORTS ONLY) WHICH IS PART OF HABARI DUNIANI MEDIA GROUP. WE ALWAYS BRING TO YOU ANALYTICAL NEWS IN YOUR FINGER TIPS. TO ADVERTISE WITH US, EMAIL US VIA habariduniani@gmail.com
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment