Abdulrahman
Mohamed, Kipa wa JKU ya visiwani Zanzibar, jana alitarajia kusaini mkataba wa
miaka miwili ya kuichezea Simba kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Uamuzi
wa kumsajili kipa mwingine ulitokana na usumbufu uliodaiwa kutolewa na kipa mkongwe
wa timu hiyo, Ivo Mapunda aliyechukua Sh10 milioni, lakini akashindwa kusaini
mkataba wa mwaka mmoja huku ikielezwa alikuwa akitoa sababu mbalimbali
alipotakiwa kwenda kusaini.
Mpaka
jana Ivo alikuwa hajasaini mkataba na timu hiyo na kuna uwezekano mkubwa wa
yeye kutemwa pamoja na kuchukua fedha hizo.
0 comments:
Post a Comment