Msimu
wa 2015/2016 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, unatazamiwa kuanza kutimua
vumbi jumamosi Septemba 12, 2015 kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja
tofauti nchini.
Ndanda FC ya Mtwara watakua
wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana
kimanumanu African Sports watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga, huku Wana Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu
katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Azam FC watakua wenyeji wa
Tanzania Prisons kaika uwanja wa Chamazi Complex, Stand United FC chama la wana
watawakaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto
Africans watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City
watacheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Jumapili Ligi Kuu itaendelea
kwa mchezo mmoja tu utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
ambapo mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga SC watawakribisha wagosi wa kaya
Coastal Union.
Ndanda FC | vs | Mgambo JKT | 16:09 |
African Sports | vs | Simba SC | 16:09 |
Majimaji | vs | JKT Ruvu | 16:09 |
Azam FC | vs | Tanzania Prisons | 16:09 |
Stand United | vs | Mtibwa Sugar | 16:09 |
Toto Africans | vs | Mwadui FC | 16:09 |
Sun Sep 13th | |||
Young Africans | vs | Coastal Union |
Katika hatua nyingine klabu ya
Kagera Sugar ya mkoani Kagera itatumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini
Tabora kwa mechi zake za nyumbani dhidi ya Toto Africans (Sept 26), JKT Ruvu
(Sept 30), Tanzania Prisons (Oct 4) na Yanga (Oct 31).
Mabadiliko hayo yamefanyika
kupisha shughuli ya uwekaji nyasi bandia inayoendelea kwenye uwanja wao wa
Kaitaba mjini Bukoba unaofanywa na wataalamu kutoka Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA).
0 comments:
Post a Comment