AZAM FC MABINGWA WAPYA CECAFA KAGAME CUP 2015, WAIFUNGA GOR MAHIA 2-0


Timu ya Azam FC ya Tanzania imeweka historia baada ya kuchukua ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagame kwa mara ya kwanza baada ya kuwachapa Gor Mahia ya Kenya bao 2-0. Ikiwa ni timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa kombe hilo.

Mabao hayo yaliyowapa heshima Azam FC yalipachikwa dakika ya 16 na nahodha John Bocco (Boko Haram) aliyeunganisha krosi safi ya Muivory Coast Kipre Tchetche na la pili lilimaliziwa na Tchetche dakika ya 65 kwa njia ya faulo iliyokwenda moja kwa moja golini na kumshinda kipa wa Gor  Boniface Oluoch.


Katika mchezo huo, Azam FC ilicheza soka la mbinu za ushindi ikitumia fomesheni ya 3-5-2 waliipoteza kabisa Gor Mahia hasa washambiliaji wake Meddy Kagare na Michal Olunga ambao hawakufulukuta kwa ngome iliyoongozwa na Serge Wawa Pascal.

Azam FC ilifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa, Ame Ally na kumwingiza Frank Domayo dakika 46 Farid Mussa akaingia Erasto Nyonni na Tchetche alitoka akaingia Didier Kavumbagu dakika ya 86

Azam FC pia imeweka historia ya aina yake baada ya wachezaji wake kushinda tuzi za mchezaji bora kila mechi. beki wa kati, Muivory Coast, Serge Wawa 'Waziri wa Ulinzi' amekuwa mchezaji bora wa mechi tatu huku Salum Abubakar, Farid Mussa Shah na Aishi Salum Manula wakishinda tuzo hiyo mara moja kila mmoja. Kwa maana hiyo wachezaji wa Azam FC walishinda tuzo za mchezaji bora wa mechi kwenye kila mchezo.


Kivutio kingine ni kwa Serge Wawa Pascal kuwa mchezaji bora wa mashindano huku mlinda lango Aishi Manula akishinda tuzo ya  nyanda bora wa mashindano.

SOMA: Usajili wa Azam FC

Kikosi cha Azam FC

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Said Morrad,Aggrey Morris, Serge Wawa, Mugiraneza Jean Baptiste, Himid Mao, Kipre Tchetche/Kavumbagu, Ame Ally/Frank Domayo, Bocco,  Farid Mussa/ Erasto Nyoni.
Share on Google Plus

About Habari Duniani

WELCOME TO MICHEZOTU (SPORTS ONLY) WHICH IS PART OF HABARI DUNIANI MEDIA GROUP. WE ALWAYS BRING TO YOU ANALYTICAL NEWS IN YOUR FINGER TIPS. TO ADVERTISE WITH US, EMAIL US VIA habariduniani@gmail.com
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment