Michael Olunga |
YANGA YAPOTEZA MECHI YA KWANZA
Yanga wameanza vibaya Mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA KAGAME CUP, baada yyya kufungwa 2-1 na Gor Mahia ya
Kenya katika Mechi ya Kundi A iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Yanga walianza vyema Mechi hii kwa kupata Bao Dakika ya 4 tu baada
ya Krosi ya Straika wa Zimbabwe Donald Ngoma kukatwa na Beki wa Gor, Dirkir
Glay na kutinga wavuni.
Lakini Dakika ya 16 tu, Gor walisawazisha baada ya Frikiki ya Glay
kuunganishwa kwa kichwa na Shakava.
Balaa kwa Yanga liliendelea katika Dakika ya 25 baada Ngoma kupewa
Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Gor walipata Bao lao la Pili Dakika ya 46 kupitia Michael Olunga.
Yanga wangeweza kuambua Sare licha ya kucheza muda mrefu wakiwa
pungufu walipopata Penati Dakika ya 76 baada ya Beki wa Gor kuunawa Mpira
lakini Kepteni Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alipiga Staili ya Panenka na Kipa
Boniface Olouch kuokoa Mpira huo.
VIKOSI:
KIKOSI CHA YANGA
Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul [Joseph Zuttah, Dakika
ya 75], Mwinyi Haji, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Simon
Msuva [Kpah Sherman, 69], Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Donald Ngoma, Deus
Kaseke [Salum Telela, 84]
KIKOSI CHA GOR MAHIA
Boniface Olouch, Mussa Mohammed, Sibomana Abouba, Harun
Shakava, Kari Nzigiyimana, Dirkir Glay, Khalid Aucho [Erick Ochieng, Dakika ya
89], Godfrey Walusimbi [Ronald Omino, 86], Innocent Wafula [Enock Agwanda, 86],
Medie Kagere, Michael Olunga.
0 comments:
Post a Comment