Waimbaji
wa Kundi la Olalang, ndio kundi litakalomburudisha rais Obama atakapozuru
Kenya.
Kundi hilo la Kimaasai kutoka
mji wa Maasai Mara nchini Kenya limeandaa nyimbo na densi za kimaasai tayari
kabisa kukonga moyo wa kiongozi mwenye nguvu zaidi duniani.
Kundi hilo linalowajumuisha
wanaume na wanawake kutoka jamii ya maasai limekuwa likifanya mazoezi kwa zaidi
ya miezi mitatu tangu lilipoarifiwa kuwa litamtumbuiza rais Obama.
Mkurugenzi
wa kundi hilo, Gideon ole kitare, anasema kuwa wanafurahia kuchaguliwa kumpokea
mgeni wa hadhi ya Rais Obama.
‘Hii ni mara yetu ya kwanza
kuwa katika ngazi ya kimataifa na tunatarajia kuwa itakuwa ni fursa kubwa
kuonekana na wageni kutoka nchi za nje na hata kualikwa kuandaa burudani nje ya
nchi.
Hata hivyo, kundi hili ni la
densi maalum kwa Rais Obama kinyume na densi za kawaida.
James Ole Kar Kar, mmoja wa
waimbaji wa kundi hili, anasema kuwa wamejumuisha nyimbo na densi maalum za
kimaasai kwa sababu ya rais Obama.
‘’Tumemuandalia wimbo unaoitwa
''Orkonti'' ambao ni wimbo wa kumkaribisha shujaa kama Rais Obama.’’
‘’Wimbo huo ni wa kumpa nguvu
shujaa ili aweze kuwa na uwezo wa kufanya mambo muhimu.’’ Aliongeza
0 comments:
Post a Comment