Pierre-Emerick Aubameyang mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya
Gabon na klabu ya Borrussia Dortmund ya Ujerumani, ndio mchezaji bora wa mwaka
2015.
Aubameyang mwenye umri wa miaka 26 alipewa tuzo hiyo jijini Abuja
jana usiku baada ya kupata alama 143 mbele ya mshambuliaji wa Manchester City
na Cote Dvoire Yaya Toure aliyepata alama 136.
Mbwana Samatta kushoto na Pierre-Emerick Aubameyang kulia |
Aubameyang anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Gabon kuwahi kushinda
taji hili baada ya kupigiwa kura na makocha pamoja na wakurugenzi wa kiufudi
kutoka barani Afrika.
Mshambuliaji huyo wa Borrussia Dortmund anaongoza kwa ufungaji wa
mabao katika ligi ya Bundesliga msimu huu ,na kati ya mechi 17 alizocheza
amefunga mabao 18.
Kwa upande wa wachezaji wanaocheza soka katika vlabu vya bara
Afrika, Mtanzania Mbwana Samatta aliyekuwa anaichezea klabu ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameshinda tuzo ya mchezaji bora na anakuwa
Mtanzania wa kwanza lakini pia kutoka Afrika Mashariki kunyakua taji hili.
0 comments:
Post a Comment