MAOMBI YASIMAMISHA MECHI NA BURUDANI ZAMBIA

Zambia. Mechi za soka nchini Zambia zilizokuwa zimepangiwa kuchezwa wikendi hii zimeahirishwa kutokana na siku ya kitaifa ya maombi Jumapili.

Rais Edgar Lungu alitenga siku hiyo kuwa ya kuomba msamaha na maridhiano, lengo kuu likiwa kuomba usaidizi kutoka kwa Mungu kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi yanayokabili taifa hilo.

Raia wameombwa kutojihusisha katika shughuli za burudani na wamiliki wa mabaa wameombwa kuyafunga siku hiyo.
Shirikisho la Soka la Zambia (Faz) limeamua kuitikia wito wa rais.

"Ni wakati wetu sote kunyenyekea tena kwa Mungu, kutia nguvu uhusiano wetu naye na kumuomba kuongoza maisha yetu, mchezo wetu na taifa letu,” mkuu wa Faz Kalusha Bwalya amesema.

Share on Google Plus

About Habari Duniani

WELCOME TO MICHEZOTU (SPORTS ONLY) WHICH IS PART OF HABARI DUNIANI MEDIA GROUP. WE ALWAYS BRING TO YOU ANALYTICAL NEWS IN YOUR FINGER TIPS. TO ADVERTISE WITH US, EMAIL US VIA habariduniani@gmail.com
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment