Mrisho Ngassa (kushoto)akiwania mpira na mchezaji wa Malawi. |
Dar es Salaam. Taifa Stars, TIMU ya Taifa ya Tanzania
imewatandika bila huruma timu ya Malawi mabao 2-0 katika mechi yao ya kuwania
kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018. Mechi hiyo na kusisimua ilichezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.
Mpira ulianza kwa Stars kulisakama lango la Malawi,
huku washambuliaji wake wakiisakama ngome ya Malawi.
Dakika ya pili Stars walikosa bao la wazi kupitia kwa
Mrisho Ngassa baada ya Thomas Ulimwengu kupiga krosi safi lakini kipa wa Malawi
Simplex Nthalaaliokoa shuti hilo.
Dakika 18 Stars waliwanyanyua Watanzania baada ya
Mbwana Samatta kufunga bao kwanza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa
Ulimwengu.
Stars waliendelea kulisakama lango la Malawi ambapo
dakika ya 22 Ulimwengu alifunga bao la pili baada baada ya kuunganisha krosi ya
Haji Mwinyi.
Dakika ya 37 Malawi walifanya shambulizi kali
mshambuliaji wao John Banda akiwa ndani ya 18 aliachia shuti kali lakini kwa
umakini wa kipa wa Stars Ally Mustapha 'Bartez' alidaka shuti hilo.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Stars walikuwa
mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Malawi kubadilika na
kucheza kwa kushambulia lakini mabeki wa Stars walikuwa makini kuokoa hatari
zote.
Dakika ya 50 almanusura Stars wapate bao la tatu baada
ya Ngassa kuachia shuti kali baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ulimengu
lakini mpira ukapita pembeni na kutoka nje.
Stars waliendelea kufanya mashambulizi ya nguvu dakika
ya 67 walikosa bao la wazi baada ya Samatta kufanya kazi kubwa na kumpa pasi
Ulimwengu ambaye mpira wake wa kichwa uligonga mwamba na kurudi ndani ambapo
mabeki wa Malawi wakawahi kuokoa.
Dakika ya 80 Malawi walikosa bao la wazi baada ya
mchezaji wake kuachia shuti kali lakini kipa wa Stars akapangua shuti hilo na
mpira kuwa kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda.
Hadi kipenga cha mwisho kinalia Stars walitoka kifua
mbele kwa mabao 2-0.
0 comments:
Post a Comment