AZAM FC YATINGA NUSU FAINALI
Azam FC imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya CECAFA Kagame Cupbaada ya ushindi wa
penalty 5-3 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
Baada
ya timu hizo kumaliza dakika 90, bila ya kufungana ndipo ilipokuja changamoto
ya mikwaju ya penalti ambayo mwaka huu imekuwa mwiba mchungu kwa Yanga ambayo
kabla ya penalti za jana tayari ilishakosa penalti tatu katika michezo ya hatua
za makundi.
Shujaa
wa Azam katika mchezo wa jana alikuwa ni kipa Aishi Manula aliyechaguliwa
mchezaji bora wa mechi baada ya kudaka penalti ya tatu ya Yanga iliyopigwa na
Haji Mwinyi.
Wachezaji
Kipre Herman Tchetche, Serge Wawa Pascal wote raia wa Ivory Coast, John Bocco,
Himid Mao na Aggrey Morris walifunga penati zao, wakati za Yanga SC zilifungwa
na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela na Godfrey Mwashiuya.
Katika
mtanange wa dakika tisini Azam FC iliutawala mchezo hasa kipindi cha kwanza na
kukosa magoli mengi kupitia kwa John Bocco, Kipre Tchetche na Shomari Kapombe.
Azam
FC sasa itamenyana na KCCA ya Uganda katika Nusu ya pili Ijumaa, baada ya
Khartoum N na Gor Mahia kupambana katika Nusu Fainali ya kwanza.
Utamu
ni kwamba, Nusu Fainali zote zitakuwa marudio ya mechi za makundi, kwanza Azam
FC iliifunga 1-0 KCCA katika mechi ya Kundi C na Khartoum N ilitoka sare ya 1-1
na Gor Mahia katika mchezo wa Kundi A.
Kikosi cha Azam FC:
Aishi
Manula, Shomari Kapombe, Agrey Morris, Abdallah Kheri/Said Mourad dk46, Paschal
Wawa, Jean Mugiraneza, Himid Mao, Frank Domayo/Ame Ally dk46, Farid Mussa, John
Bocco na Kipre Tchetche.
Yanga SC:
Ally
Mustafa ‘Barthez’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul/Joseph Zuttah dk69,
Godfrey Mwashiuya, Donald Ngoma, Kevin Yondani, Mbuyu Twite, Deus Kaseke/Salum
Telela dk61, Amisi Tambwe, Haruna Niyonzima/Malimi Busungu dk80 na Hajji
Mwinyi.
0 comments:
Post a Comment