WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA - TAIFA STARS |
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mchezo wake wa
kwanza wa kombe la COSAFA siku ya jumatatu dhidi ya Swaziland katika
uwanja wa Royal Bafokeng pembeni kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya
saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Kusini.
Awali michezo ya
kundi B ilikuwa ifanyike katika uwanja wa Olympia Park, lakini waandaji wa
michuano ya COSAFA Castle wamesema kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wao
michezo hiyo imeshindikana kufanyika katika uwanja huo.
Uwanja wa Royal
Bafokeng ni miongoni mwa viwanja viliyotumika katika Fainali za Kombe la Dunia
2010 chini Afrika kusini, ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji 42,000 huku
timu ya Platinum Stars iliyopo Ligi Kuu ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani.
Leo asubuhi Taifa
Stars imefanya mazoezi katika uwanja wa shule ya Rustenburg chini ya kocha mkuu
Mart Nooij, na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo huo
wa jumatatu.
Kesho jioni Taifa
Stars ifanya mazoezi saa jioni katika uwanja wa Rolay Bafokeng kwa ajili ya
kuuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe dhidi ya Swaziland.
Akiongelea hali ya
hewa, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea
kuizoea hali ya hewa, japokuwa kuna baridi hakuna mchezaji aliyeshindwa kufanya
mazoezi kutokana na hali ya hewa.
NB: Picha za mazoezi
ya Taifa Stars zimeambatanishwa
IMETOLEWA NA
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment